Nairobi : wadau wa mzozo wa Kongo wanakutana pasina kujumulisha M23

Nairobi : wadau wa mzozo wa Kongo wanakutana pasina kujumulisha M23

Tangu jumatatu tarehe 28 novemba, wadau wa mzozo wa Kongo wanakutana mjini Nairobi kwa kipindi cha siku sita. Kundi la M23 kundi la waasi linalodhibiti maeneo mengi katika mkoa wa Kivu-kaskazini halikualikwa katika mazungumzo hayo. HABARI SOS Médias Burundi

Takriban wajumbe 200 watakuwa katika makao makuu ya Kenya kwa siku sita ili kutafuta suluhu la mzozo wa mashariki mwa Kongo, rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta amekumbusha kuwa ni raia wa Kongo wanaotakiwa kufanya nguvu ili kuokoa nchi yao.

” Mnatakiwa kuelewa kuwa suluhu italetwa na nyinyi wenyewe kama raia wa Kongo. Hakuna mtu mwingine. Sisi tuko hapa ili kuwasaidia na kuwaombea Mungu. Jukumu kubwa ni la kwenu. Mnatakiwa kujuwa kuwa mali zetu zinatakiwa kuwasaidia badala ya kuwa chanzo ya kumwaga damu yenu, amefahamisha kwa sauti kali.

Kwa mjibu wa rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye nchi yake inatuhumiwa kila Siku kuunga mkono kundi la M23, ” Sababu kuu ya kuendelea kwa mzozo huo ni kushindwa kutekeleza makubaliano mengi yaliofikiwa kwa ngazi na nyakati tofauti miaka iliyopita. Natumai kuwa safari hii juhudi hizo zitaleta matunda mazuri”.

Rais wa Kongo upande wake anasema ni fursa kubwa ambayo” inatakiwa kuchukuliwa “. Félix Tshisekedi amelinganisha hali ya mashariki ya nchi yake na “Kuzama”

” Hapa na kwa sasa, tunatakiwa kuwajibika kwa kasi na katika muungano ili kuondoa mikoa ya Ituri, Kivu kusini na kaskazini, Tanganyika kutoka kile ninachoita mzamo. Tunatakiwa kuzimisha silaha mara moja ili kutoa fursa kwa mpango wetu wa pamoja wa kujenga upya nchi yetu” , alisema bwana Tshisekedi.

Rais wa jamuhuri ya Burundi ambaye pia ni mwenyekiti wa jukwa la ma rais wa EAC amewaomba mahasimu kuchukulia mfano wa warundi na makubaliano ya Arusha yaliyotiwa saini mwaka wa 2000.

” Nchini Burundi, kulikuwa na takriban makundi kumi. Tulikuwa na vyama kumi na saba vinavyohasimiana lakini wakati kanda iliposimama, warundi walikaa pamoja na walipata amani. Msipoteze matumaini. Mkikubali kukaa pamoja na kuongea kwa uhakika, mtapata amani” amesisitiza rais Neva aliyezindua awamu ya tatu ya mazungumzo ya Nairobi.

Kundi la M23 halikualikwa kwenye mazungumzo hayo, amethibitishia SOSMedias Burundi msemaji wa kundi hilo.

[….] matokeo ya mazungumzo hayo yanawahusu wale walioalikwa. Sisi tunaendelea kumuomba mpatanishi atupokeye na asikilize madai yetu. Tunasubiri zamu yetu ‘ amebaini Munyarugero Karemera Canesius, msemaji wa kundi la M23.

Na kuzidi ” kuhusu mapigano, tulisimamisha mapambano mara baada ya tangazo la wakuu wa nchi katika mkutano wa Luanda (Angola). Tuliheshimu uamzi huo. Kile tunachoendelea kuomba ni kwamba serikali ya Kinshasa isimamishe kutushambulia wakati tukisubiri matokeo ya mazungumzo “.

Angalau makundi 40 ya waasi yalialikwa mjini Nairobi. Lakini wajumbe wa mashirika ya kiraia na makundi ya silaha ya kivu-kusini wamekwamia Goma, makao makuu ya mkoa wa Kivu-kaskazini.

Wanasema kutojuwa sababu za mkwamo huo na kudai kuwa haiwezekani mazungumzo yaendelea pasina wao ” kushiriki”

Mbali na ma rais wa Burundi na Kenya, viongozi wengine wa jumuiya ya afrika mashariki wamefuatiliwa uzinduzi wa mazungumzo hayo kupitia video.

Previous Karusi: a man admitted after being stabbed by an Imbonerakure
Next Tanzania: Malnutrition-related diseases threaten under five children in Burundian refugee camps