Burundi : watetezi wanne wa haki za binadamu wanashikiliwa na idara ya ujasusi ndani ya jiji kuu la kibiashara Bujumbura

Burundi : watetezi wanne wa haki za binadamu wanashikiliwa na idara ya ujasusi ndani ya jiji kuu la kibiashara Bujumbura

Maafisa wa SNR (idara ya kitaifa ya ujasusi) wamewakamatwa wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura jumanne hii wakijiandaa kuwasili mjini Kampala ( mji mkuu wa Uganda) kushiriki kwenye mkutano. Waranti wa muda wa kuwakamatwa umetolewa lakini viongozi tawala hawajafahamisha sababu za kukamatwa kwao. HABARI SOS Médias Burundi

Watu hao ni akinamama watatu na mwanaume mmoja: Audace Havyarimana muwakilishi wa shirika kwa ajili ya amani na kuendeleza haki za binadamu (APDH), Sylvana Inamahoro, meneja mtendaji wa shirika hilo, Sonia Ndikumasabo kiongozi wa shirika la akinamama wanasheria ( AFJB) pamoja na Marie Emerusabe mratibu mkuu wa shirika hilo.

” Wamesimamishwa asubuhi hii kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura na kupelekwa moja kwa moja katika gereza la idara ya ujasusi ndani ya mji huo” vyanzo vya karibu na faili hiyo vimeripoti.

” Idara ya SNR kupitia sauti imehakikishia CNIDH (tume huru ya kitaifa ya haki za binadamu) kuwa uchunguzi umefunguliwa dhidi ya wajumbe hao wanne wa mashirika “, vyanzo tofauti vimearifu jumanne hii usiku.

Kwa mjibu wa vyanzo vyetu, waranti wa kukamatwa kwao huenda umetolewa na mwendeshamashtaka.

” Sio mara ya kwanza kwa watetezi hao wa haki za binadamu kuelekea katika mji mkuu wa Uganda kwa ajili ya majukumu ya kazi yao. Haieleweki kuona leo wamekamatwa”, vyanzo vyetu vimearifu.

Mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri Sylvestre Nyandwi pamoja na msemaji wa korti kuu Agnès Bangiricenge hawakupatikana ili kujieleza juu ya taarifa hizo.

Wizara ya sheria nchini Burundi, halijatoa tangazo lolote kuhusiana na hali hiyo.

Katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Burundi, Eamon Gilmore mjumbe maluum wa umoja wa ulaya kwa ajili ya haki za binadamu alifahamisha kuwa ” bado kuna changamoto katika maswala ya haki za binadamu nchini”.

Mmoja kati ya hao wanaozuiliwa jela ambaye ni Sonia Ndikumasabo, aliwahi kuwa naibu mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya haki za binadamu.

Anchaire Nikoyagize, kiongozi wa shirika la Iteka, shirika la zamani la kutetea haki za binadamu ndani ya nchi hiyo ndogo ya afrika mashariki amethibitisha taarifa hizo za kuzuiliwa kwa watetezi hao wanne wa haki za binadamu bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Previous Burundi : four human rights defenders detained by intelligence in the commercial city of Bujumbura
Next Rwanda-DRC: the Rwandan army announces that it has repelled an aggression by Congolese soldiers