Burundi : vinywaji vya Brarudi kupanda bei

Burundi : vinywaji vya Brarudi kupanda bei

Tangu jumapili 16 oktoba, vinywaji vya Brarudi (Kiwanda cha kutengeneza vinywaji nchini Burundi) vilipandishwa bei. Bei ilipanda kati ya franka 200 na 700 kwa chupa moja. Wanunuzi wanalaani kuwa bei imepanda kwa kiwango kikubwa katika nchi hiyo ambako uwezo wa wanunuzi unazidi kushuka.
Wanaomba serikali kutumia ushawishi wake ili kustaawisha bei ya vinywaji vya Brarudi. HABARI SOS Medias Burundi

Bei mpya zilitangazwa kupitia tangazo la kiwanda cha Brarudi siku ya jumapili.

[….] Soda zitaanza kuuzwa kwa franka 1000 sarafu za burundi.
Chupa la biya maarufu Nyongera na aina ya Primus ndani ya chuma dogo bei yake ni 1200 badala ya 1000 sarafu za burundi. Pombe aina ya Primus kubwa bei yake imetoka kwenye 1500 hadi 1700 wakati ambapo Amstel ya ndani ya chupa kubwa, bei yake ilikuwa 1900 sasa itakuwa 2500 sarafu za burundi. Chupa dogo nalo bei itakuwa 2100 badala ya 1500.
Bei ya pombe aina ya Royal sasa ni 2600 wakati bei ya awali ilikuwa 2200 sarafu za burundi. Kwa wapenzi wa pombe ya Amstel bock watakuwa wanalipa pesa 2100 badala ya 1400 sarafu za burundi, yanasomeka katika tangazo hilo.
Mpangilio mpya wa bei ya vinywaji vya Brarudi ulitangazwa rasmi baada ya ujanja mwingi katika biashara ya vinjwaji vya kiwanda hicho cha zamani kabisa.
Uhaba wa vinjwaji hivyo umekuwa ukishuhudiwa na kusababisha wasi wasi mkubwa kwa watumiaji wa bidhaa hiyo. Wanalaani ongezeko hilo la bei kwa kiwango kikubwa katika nchi hii ambapo uwezo wa wanunuzi unazidi kushuka chini.

Wakaazi wa jiji la Bujumbura na wamiliki wa kilabu vya pombe wapata hofu.

” Brarudi imeweka viwango vya juu. Tuchukuwe mfano wa pombe ya Amstel chupa kubwa, wanunuzi warundi hawawezi kumudu bei yake”, analalamika mmiliki wa kilabu.

Walanguzi wadogo upande wanasema kuhofia ” kutokuwa na mtaji wa kutosha ili kujaza ghala zao.

wakaazi wanaomba serikali kuingilia kati na kustaawisha bei ya vinywaji vya Brarudi kwa kuzingatia hali ya kijamii na uchumi wa nchi.

Previous Rumonge: water shortage
Next Photo of the week: five thousand expropriated households ask for relocation