Kivu-kaskazini: Mapigano kati jeshi la FARDC na M23 yaibuka katika eneo la Rutshuru

Kivu-kaskazini: Mapigano kati jeshi la FARDC na M23 yaibuka katika eneo la Rutshuru

Mapambano mapya kati ya jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo (FARDC) na kundi la M23 yalianza tangu ijumaa asubuhi katika vijiji vingi vya wilaya ya Rutshuru katika mkoa wa Kivu ya kaskazini, mashariki mwa DRC. Vyanzo eneo hilo vinasema kuwa risasi zilisikika na milio ya silaha za kawaida na nzito. Makabiliano hayo wanaendelea katika eneo hilo la Kongo, vyanzo vya habari vinaendelea kusema. HABARI SOS Médias Burundi

Hali ya wasi wasi ilishuhudiwa katika vijiji na maeneo ya wilaya ya Rutshuru ambapo wananchi wanakimbia mapigano na kuelekea kwenye makao makuu ya Rutshuru. Wengine wanakwenda nchini Uganda.
Vyanzo vyetu vinataarifu kuwa hadi jumapili hii mapigano yameendelea katika vijiji vya Rangira na Rwanguba.

” Kundi la M23 limeshambulia ngome za jeshi letu la FARDC eneo la Rangira-Rwanguba. Wako katika milima ya Shwema. Wanapiga mabomu kwenye baadhi ya ngome zetu. Wamefanya hivyo tangu saa tisa. Jeshi la FARDC linajihami. Wako wanashambulia kwa mabomu milima hiyo, aliwambia wandishi wa habari Jean Claude Mbabanze kiongozi wa mashirika ya kiraia hapo Rutshuru.

” Hadi sasa jeshi la FARDC liko katika hali nzuri. Kundi la M23 haijaweza kusonga mbele angalau mita moja. Tangu waliposikia kuwa hapatakuwa mazungumzo, wanasikitika. Wanataka kuilazimisha serikali kuzungumza nao. Wanadhani ili yafanyike mazungumzo ni lazima wafunge barabara RN2( Barabara ya kitaifa namba mbili) ya Goma-Rutshuru au kuuteka mji wa Rutshuru ili kushinikiza” , alizidi kusema.

Raia mmoja aliuwawa na mwingine kujeruhiwa katika mapigano hayo kulingana na vyanzo vyetu eneo hilo.

Katika tangazo, kundi la M23 linafahamisha kuwa ngome zake eneo la Rutshuru zimeshambuliwa na muungano wa makundi mengi ya wapiganaji ya ndani na nje ya nchi yakiwemo makundi la Mai Mai na FDLR.

Kundi hilo la mwezi machi tarehe 23 linafahamisha kuwa limejihami. Wanalaani kuona viongozi tawala wa Kongo wamekataa kufanya mazungumzo na kundi hilo ili kumaliza vurugu mashariki mwa Kongo licha ya ushahuri wa UN, wakuu wa nchi za ukanda na umoja wa afrika.

Ma mia ya wananchi wa kawaida wanaendelea kukimbilia nchini Uganda, walishuhudia hayo wandishi katika maeneo hayo.
Jeshi la FARDC wamedai kudhibiti maeneo yaliyokuwa yanashikiliwa na kundi la waasi wa M23 jambo ambalo halijakubaliwa au kupingwa na kundi hilo linalodhibiti mji wa mpakani wa Bunagana tangu tarehe 13 juni mwaka huu.

Previous Gitega: discovery of two dead bodies
Next Photo of the week - Bubanza : former MP Fabien Banciryanino sparks controversy