Gitega: bei ya bidhaa za vyakula imepanda hadi mara mbili, wananchi wana wasi wasi

Gitega: bei ya bidhaa za vyakula imepanda hadi mara mbili, wananchi wana wasi wasi

Wakaazi wa jiji kuu la kisiasa (kati kati mwa Burundi) wanasema kuzidiwa na kupanda kiholela kwa bei ya nafaka za vyakula. Baadhi ya bidhaa za vyakula bei imepanda takriban mara mbili. Viongozi tawala wanawatuhumu wafanyabiashara kupandisha bei, huku upande wao wakidai kuwa ni kutokana na thamani ya pesa ilyoporomoka. HABARI SOS Médias Burundi

Nafaka za vyakula kwa jumla zote zimepanda bei. Wakaazi wanasema kuwa wameshindwa kumudu bei hiyo.
” Bei ya kilo moja ya maharagwe ya kawaida na aina nyingine maarufu kinure iliokuwa 1500 hadi 1900 sasa ni 1800 hadi 2200 sarafu za Burundi. Bei ya mchele imepanda kwa kiwango cha elfu moja kwa kila aina ya mchele. Mchele wa bei kubwa ni ule maarufu mtanzania ambao bei ni 4500 sarafu za Burundi kilo moja” wakaazi wanasema.

Hali ya kupanda kwa bei umeshuhudiwa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Wanazidi kuwa hata bei ya viazi ulaya ambavyo kawaida bei yake iko chini, sasa imepanda kutoka 900 hadi 1200 kilo moja, maharagwe, mihogo, unga, ndizi […] vimeshuhudia pia bei kupanda kiholela kwenye soko.

Mkuu wa kijiji cha Gitega anawatuhumu wafanyabiashara kupandisha kwa kutaka bei ya bidhaa za vyakula, lakini wanakanusha vikali madai hayo. Wanasema bei inapanda kutokana na kupoteza thamani kwa sarafu ya Burundi.

Pamoja na maelezo hayo, wakulima wanafikiria kuwa bei imepanda kutokana na mavuno kupungua hali ambapo wanazidi kusema ilitokana na ukosefu wa pembe jeo kwa wakati ikiwemo mbolea ya FOMI (kiwanda cha kutengeneza mbolea ya kizungu) pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkuu wa kijiji cha Gitega anafahamisha kuwa kamati ya kudumu yenye jukumu la kufuatia bei imeundwa.
” Mfanyabiashara ambaye atapandisha bei ataadhibiwa” alitahadharisha.

Katika mikoa mingine ya nchi hiyo ndogo ya afrika mashariki kama Bubanza na Cibitoke (Kaskazini-magharibi mwa nchi) wakaazi wanasema kuwa hawawezi tena kumudu gharama za maisha.

Previous Gitega: the price of food products goes up to double, residents are worried
Next Nakivale (Uganda) : WFP updates its data