Rwanda: wakimbizi wa Kongo walalamika mbele ya ubalozi tofauti mjini Kigali

Rwanda: wakimbizi wa Kongo walalamika mbele ya ubalozi tofauti mjini Kigali

Wawakilishi wa zaidi ya wakimbizi 70.000 kutoka Kongo wanaopewa hifadhi nchini Rwanda waliwasilisha waraka kwenye balozi tofauti mjini Kigali jumatatu hii tarehe 23 januari ili kufahamisha jamii ya kimataifa kusaidia katika kumaliza mauwaji na mateso dhidi ya jamii ya watutsi wa mashariki mwa Kongo. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa sehemu kubwa ni raia wa Kongo watumiaji wa lugha ya Kinyarwanda wenye asili ya mikoa ya Kivu kaskazini na kusini. Wanahakikisha kuwa lengo laao ni kuifanya jamii ya kimataifa kuwa shahidi ya usalama mdogo nchini DRC. Wanaomba pia kuwarejea kwa amani ndani ya nchi yao. Wakimbizi hao ambao baadhi yao walimaliza miaka 25 ndani ya kambi, wanasema kuwa wanafohia kuwa ” watu wasiokuwa na uraia wowote”.

Wananchi hao wa Kongo wameweka waraka wao kwenye ubalozi wa Ufaransa, uholanzi, ubelgiji na Uganda mjini Kigali. Wana mpango wa kujielekeza kwenye ubalozi mwingine.

Waraka huo umetungwa siku chache baada ya kufanya mandamano ya amani dhidi ya ghasia za kikabila zinazochukuliwa kama mauwaji ya halaiki ndani ya mkoa wa Kivu kaskazini na Kivu kusini mashariki mwa DRC.

Waraka huo pia umefuata barua nyingi ne ya jamii ya wakimbizi wa Kongo nchini Kenya ambayo wiki iliyopita ilikabiidhiwa wajumbe wa umoja wa mataifa , umoja wa ulaya, umoja wa afrika pamoja na ubalozi wa marekani, na ufaransa jijini Nairobi.

” Hali mashariki mwa DRC inaendelea kuwa mbaya zilishuhudia nchi zilizopewa waraka huo”. amewambia wandishi wa habari John Nsengiyera mmoja kati ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi ya Kigeme katika kanda ya Nyamage, kusini mwa Rwanda.

Hata kama tunazunguza leo, ndugu zetu waliosalia nchini DRC wanaendelea kuuwawa huku wengine wakipokelewa kama wakimbizi wanaoingia nchini Rwanda. Sababu moja tu ya kuwatesa ni kabila lao la wa tutsi”, alizidi Nsengiyera.

” tunaomba jamii ya kimataifa kutoa majibu kuhusiana na malalamiko wa watu wa jamii ya watutsi wa Kongo husasan swala la kutaka kuwafanya watu wasiokuwa na taifa na kulinda raia wa Kongo watumiaji wa Kinyarwanda dhidi ya ubaguzi. Tunaomba pia ufanyike mpango wa dharura wa kuwarejesha makwao raia wa Kongo wanaoishi katika ukanda huu”, alisema.

“Zaidi ya makabila 450 yanapatikana nchini Kongo. Lakini haieleweki kwa nini kundi moja la watutsi likilengwa na mauwaji ya kikabila, unyanyasaji ya kijinsia kwa ushirikiano na jeshi la serikali “, alifahamisha Bosco Maniragaba mmoja kati ya wawakilishi wa wakimbizi katika kambi ya Nyabiheke katika kanda ya Gatsibo.

Kupitia barua hiyo, wanaomba kuteketezwa kwa makundi haramu hususan kundi la FDLR linaloundwa na waliofanya mauwaji mwakab 1994 dhidi ya watutsi nchini Rwanda na vizazi vyao.

” FDLR walitoka Rwanda lakini walitufukuza kutoka ardhi ya mababu zetu”, walilalamika wawakilishi wa jamii raia wa Kongo wanaotumia lugha ya Kinyarwanda wakimbizi nchini Rwanda.

Kwa mjibu wa wawakilishi wa wakimbizi kutoka Kongo wa kabila la watutsi wanaoishi katika kanda hii” kurejea kwa amani mashariki mwa Kongo ndio sharti kwa ajili ya kuwarudisha makwao”.

” Watoto wetu waliozaliwa ukimbizini sasa wana miaka 27 na wanaendelea kuomba haki ya kuwa na uraia”, wanasisitiza huku wakikanusha ushawishi wa Kigali katika utaratibu wao.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya maziwa makuu ya afrika unaendelea kuzorota tangu kuibuka tena kwa kundi la machi 23, M23.

Kundi hilo la zamani la watutsi lilichukuwa tena silaha mwishoni mwa 2021 likituhumu viongozi wa Kongo kushindwa kutekeleza ahadi zake za kurejesha wapiganaji wake ambao ni jamii ya watutsi wa Kongo katika maisha ya kawaida.

Viongozi wa Kongo wanakubaliana kuwa kundi hilo linapata usaidizi kutoka Rwanda, madai ambayo Rwanda inayotupitia mbali.

Previous Rwanda: more than 3,000 new Congolese refugees received
Next Kirundo: a woman found hung in her room