Burundi : Ndabirabe na tathmini yake ya sera za kiuchumi na kisiasa

Burundi : Ndabirabe na tathmini yake ya sera za kiuchumi na kisiasa

Kuna video mbili zilizotoka wiki moja iliyopita na kupata umarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini Burundi. Muheshimiwa Gélase Ndabirabe spika wa baraza la bunge la Burundi kupitia video hizo alituelimisha kuhusu maswala ya uchumi na siasa za kimataifa hadi kudai kuwa ” watu wa ulaya wanakufa na njaa” na kuomba mshikamano kwa ajili ya wakaazi wa bara hilo ” kila mwananchi wa Burundi angetakiwa kuchangia vyakula kwa ajili ya kwenda kuwasaidia wakaazi wa ulaya wanaokabiliwa na baa la njaa”. HABARI SOS Médias Burundi

Muda mfupi kabla ya kutolewa video hiyo ya sekunde 30 ambamo alionekana kuwahutubia watu, video nyingine ilisambaa tarehe 18 februari iliyopita wakati wa kazi za maendeleo ya umaa tarafani Matondo katika mkoa wa Kayanza ( kaskazini mwa Burundi) ikimuonyesha akitoa mafunzo kuhusu sera za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.

Mwenye sifa zake ya kusema uongo na kwa heshima zake za kuwa spika wa baraza la bunge, msomi huyo mwenye asili ya mkoa wa Kayanza, hakusita kusema kuwa “watu wanakuja kufanya biashara nchini Burundi sababu thamani ya sarafu ya Burundi ni ya juu ukilinganisha na nchi zingine za ukanda huu, hata na dola na euro zinapigwa chini ya sarafu ya Burundi”.

Pamoja na hayo, dola moja, chenji yake ni franka za Burundi 3780 kwenye soko la kubadili pesa lisilo rasmi na nchi ya Burundi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa sarafu za kigeni.

Kwa mjibu wa “Ndasubiramwo kwa jina lake maarufu au “wewe”, uhaba wa mafuta ya gari ambayo yamekuwa bidhaa adimu nchini Burundi katika uhalisia wa neno hilo umetokana na kwamba watu hao wa ulaja huagiza mafuta kutoka kwetu”. Jameni tangu lini Burundi inapeleka mafuta nje ya nchi?

Alikwenda mbali akifafanulia umati huo uliokija kumusikiliza msomi huyo na kusema kwamba : ” wazungu wana lengo la kutudidimiza chini ya amri zao na kutuzuia kufanya kile ambacho tunaweza kufanya na kutukubalisha kuwa tuko maskini”.

Na kumalizia yote hayo kwa kusema kuwa” kula nyama ya sungura kwa raia wa Burundi ndio matokeo na msingi wa kustawisha sarafu ya Burundi “, kwa mjibu wa kiongozi huyo mashuhuri wa bunge la Burundi.

Yakinukuliwa katika mtandao wa Twitter nchini Burundi, matamshi hayo ya Ndabirabe yalichukuliwa kama matamshi ya kisiasa na propaganda. Ukweli kwenye masoko mbali mbali ya bidhaa za vyakula kwa mfano, unaonyesha kinyume na matamshi hayo.

Kwenda kuimba mbele ya muendesha taxi anayefanya kazi hiyo ya uchukuzu kwa ajili ya kulisha familia na ambaye amemaliza siku tatu mbele ya kituo cha mafuta akisubiri bidhaa hiyo bila mafanikio na kumuambia kuwa Burundi inatuma mafuta nje ya nchi ni dalili kuwa viongozi wetu hawafahamu ukweli wa jamii ambapo wanaishi.

Ni kumuambia maneno hayo mkaazi wa mkoa wa Kayanza, moja kati mikoa inashuhudia kiwango kikubwa cha watoto wanaozaliwa ambapo wakaazi waliamuru kupeana zamu ili kulima ardhi zao ambapo pia kula mara moja kwa siku ni bahati katika mkoa huo ambapo watoto zaidi ya elfu tano waliacha shule kutokana na umasikini ndani ya familia zao katika awamu ya kwanza ya mwaka huu wa shule unaoendelea.

Previous Kivu-kaskazini : akinamama zaidi ya mia moja walibakwa na waasi wa M23 (mashirika ya kiraia)
Next Vugizo: a young girl's lifeless body discovered